Jiamini, Wewe Ni Bora, Uwepo Wako Hapa Duniani Una Umuhimu Mkubwa Sana Kwa Wanaokuzunguka, Hata Akitokea Mtu Akakudharau Usihuzunike Na Kujiona Huwezi, Kuna Watu Wanakuangalia Wewe Kama Tegemeo Lao.
Kuna Watu Wanakutazama Wewe Kama Mfano Wao Wa Mafanikio Pamoja Na Wewe Kujiona Kama Ni Binadamu Usiye Na Lolote, Hicho Kidogo Unachokifanya Kwa Wengine Ni Kikubwa Sana.
Hakikisha Haitokei Siku Ukampa Mtu Mwingine Nafasi Ya Kukupangia Maisha Ya Kuishi, Hakikisha Haitokei Siku Ukayumbishwa Na Mtu Kisa Mapenzi, Pesa Au Undugu Mlionao.
Mtu Pekee Asiyeweza Kuwa Shujaa Ni Maiti, Kama Bado Unavuta Hewa Ya Hii Dunia Basi Unaweza Kuwa Shujaa Wa Maisha Yako Na Ya Wengine, Ni Maamuzi Tu Na Kumweka Mungu Mbele, Amua Sasa, Unaweza!





Mpende jirani ni kanuni ambayo wote tunaweza tukaitumia katika maisha yetu ya kila siku, kazini,shuleni, nyumbani na katika familia zetu, hisia za huruma ni nguzo na kipande cha jamii iliyo njema.
Imani hukamata mamilioni ya watu na kufanya vitu sahihi katika jamii, imani yetu inatutaka tumpende kila mmoja wetu bila kubagua rangi,jinsia,dini,kabila au chochote kile kwani watu wote ni sawa mbele za Mungu.

INEQUALITY



Inequality is as well the issue of different set of rules for the Poor and that for the Rich. Tax havens is a clear reality about the rich being able to manipulate the tax systems of countries and the poor being left with the biggest tax burden.
If you are interested in global inequality and hence future of democracy, you should participate in addressing the plight of tax havens.
30% of Africa's financial wealth is held in tax havens while majority of Africans are languishing in deep poverty. This is an ugly face of INEQUALITY


Kufungamanisha Sekta ya Viwanda na Sekta ya Kilimo
Mheshimiwa Spika, adhma ya nchi yetu kuwa ya Viwanda ni adhma yetu sote. Jambo hili ni jambo la Maendeleo na halina ushabiki wa kivyama. Tumepitisha Mpango wa Maendeleo katika Bunge hili na kwa hiyo ni Mpango wa Nchi sio mpango wa vyama tena. Hivyo sote kwa pamoja tunafanya kazi ya kuhakikisha tunafikia malengo. Sisi tulio kwenye upinzani jicho letu pamoja na kushauri na kupendekeza ni kukosoa pale ambapo walio kwenye Serikali wanakosea. Kukosoa ni tendo la kizalendo na walio Serikalini wawe tayari kukubali kukosolewa ili kuboresha zaidi. Kwa maoni yangu, kama tusipofanya marekebisho ya kimkakati mapinduzi ya Viwanda itakuwa ni nyimbo na ngonjera za kisiasa. Watakaoumia ni Wananchi ambao hawatapata ajira na Serikali yenyewe itakosa kodi kuweza kutoa huduma kwa wananchi. Kama nilivyosema hapo awali Serikali inahitaji kufanya uratibu ili kufikia malengo. Sekta ya Viwanda au Maendeleo ya Viwanda yanapaswa kufungamanishwa na sekta nyengine za uchumi kwa sababu kuna kutegemeana. Kwa Tanzania unahitaji Sekta ya Kilimo inayokua kwa kasi ili kuzalisha malighafi kwenye viwanda. Sekta nyingine kama Elimu, Afya, Nishati, Mazingira nk zinahusiana na Viwanda pia. Kwa leo tutazame Sekta Kilimo na Viwanda kwa muktadha wa Hotuba ya Waziri wa Viwanda na kulinganisha na Hotuba ya Waziri wa Kilimo.
Mheshimiwa Spika, Sekta ya Viwanda na Sekta ya Kilimo kwa pamoja zinachangia nusu ya Pato la Taifa ( GDP) na nusu nyingine ni sekta ya Huduma. Nadharia za Uchumi zinatuambia kuwa Tija ikiongezeka kwenye ya Kilimo inawezesha sekta ya Viwanda kukua na kisha sekta ya Huduma. Hapa Tanzania nan chi nyengine nyingi za Afrika, sekta ya huduma iliruka hatua hizi na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa sana kwenye Pato la Taifa. Ndio maana tuna kitandawili nchini kwetu kuwa Uchumi unakua lakini umasikini haupungui; ni kwa sababu sekta ya huduma haijiri watu wengi kama sekta ya Kilimo na hivyo uchumi unaokuzwa na sekta ya huduma ni nadra kuondoa umasikini. Tanzania bado inapambana na umasikini. Juhudi zote tunazofanya lengo lake ni kuondoa umasikini kwa watu wetu. Sekta za kuondoa umasikini ni Kilimo na Viwanda hivyo lazima mikakati ya Serikali iendane na kufungamanisha haya. Ndio Maana Nchi nyengine Wizara ya Kilimo hujumuisha uongezaji thamani ( Ministry of Agriculture and Agro-processing ). Hatuhitaji kufanya hivyo, tunachohitaji ni kufungamanisha. Hata hivyo Serikali imeshindwa kufanya hivyo katika mwaka wake wa kwanza tu wa Bajeti. Nitaeleza kwa kutumia changamoto tuliyonayo kuhusu Sukari, Mafuta ya Kula na Nguo.
Mheshimiwa Spika, Malengo ya Serikali kwenye Viwanda yapo uk.140 ibara ya 191 ya Hotuba ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Serikali imepanga kutekeleza mambo 9 na katika mambo yote hayo hakuna hata moja linalohusiana na Viwanda vya kuzalisha bidhaa zinazohudumiwa na wananchi wengi zaidi kama Sukari na Mafuta ya kula. Bidhaa hizi ni bidhaa zinazoleta maneno ya kisiasa ndani ya nje ya Bunge. Nadhani baada ya madawa ya kulevya, bidhaa zenye mizengwe mingi zaidi katika duru za kisiasa ni Sukari na Mafuta ya kula. Sukari na Mafuta ya kula imeangusha Mawaziri kadhaa hapa nchini katika kipindi cha miaka 20 iliyopita. Hata hivyo Wizara ya Viwanda na Biashara haina mkakati kabisa kushughulika na Bidhaa hizi licha ya uwezo wake wa kutenegenza ajira na kuokoa fedha za kigeni kuziagiza. Wizara imezungumza kuhusu viwanda vya nguo lakini haijafafanua changamoto kubwa zinazoikabili sekta ya nguo nchini na hasusan biashara haramu ya magendo ya Nguo inayoathiri sana ukuaji wa sekta ya nguo nchini.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo, ukitazama hotuba ya Waziri wa Kilimo ambayo Bunge lako tukufu limeshapitisha bajeti yake kuna ‘mikakati’ ya kulima Miwa kwa ajili ya Sukari. Ukurasa wa 44 ibara ya 107 ya Hotuba ya Wizara ya Kilimo na ukurasa wa 25 ibara za 63 na 64 zinaeleza ‘mikakati’ ya kukabiliana na uhaba wa Sukari nchini. Kiambatanisho namba 6 cha Hotuba hiyo kimeeleza kwa kina changamoto nzima ya Sukari na miradi ianyopaswa kutekelezwa ili kumaliza kabisa suala la uhaba wa Sukari nchini. Nimejumlisha miradi ile kutoka kona mbalimbali za nchi na nimekuta ni takribani Hekta 300,000 za kulima Miwa. Kwa Hesabu ya chini ya wastani wa kuzalisha Sukari kwa kila Hekta, miradi hii ikitekelezwa Tanzania itaweza kuzalisha Tani 1.5 milioni za Sukari. Ukiondoa Sukari tunayotumia nchini, ziada itakayouzwa nje inaweza kuliingizia Taifa Fedha za Kigeni USD 500 milioni, sawa na 30% ya malengo ya Mpango wa Maendeleo kwa sekta ya Viwanda katika mapato ya Fedha za kigeni ya USD 3bn. Hapo sijaeleza kiwango cha Ajira kitakachopatikana, ukuaji wa biashara kwenye sekta nyengine na Umeme utakaozalishwa ( Multiplier effect ).
Mheshimiwa Spika, swali la kujiuliza, chukulia Wizara ya Kilimo inalima hiyo miwa hekta 300,000 halafu Wizara ya Viwanda haina mpango wa hivyo viwanda, hii miwa itakwenda wapi? Sio kwamba inapaswa kufungaminisha Kilimo cha Miwa na Viwanda vya Sukari? Ni kwa nini Wizara 2 zilizo chini ya Serikali moja zinashindwa kusomana? Baraza la Mawaziri linajadili nini? Ndio maana Rais anajikuta akitoa matamshi ya Mawaziri barabarani. Suala la Rais kutoa matamko kuhusu Sukari sio sawa, hii ni Kazi ya Mawaziri maana mnam expose Rais. Rais sio mtu wa kuhangaika na masuala ya kunywa Chai na Uji.
Mheshimiwa Spika, nashauri Bunge lako tukufu leo lisipitishe Bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ili Wizara hii ikakae na Wizara ya Kilimo wawianishe mipango hii na kisha walete hapa Bungeni ndio tupitishe.



Hotuba ya Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo ndg. Kabwe Z R Zitto kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama iliyoketi jijini Dar es Salaam tarehe 25 Aprili 2016 Leo tunakutana, miezi sita baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na mwaka mmoja na mwezi mmoja tangu tuzindue rasmi Chama chetu kinacholenga kujenga Ujamaa wa Kidemokrosia nchini kwetu. 
     Leo tunakutana tukikaribia mwaka mmoja tangu tuzindua Azimio la Tabora linalotaka kuhuisha Azimio la Arusha ambalo mwakani linatimiza miaka 50 tangu litangazwe na Chama cha TANU kule mjini Arusha. Tangu tulipokutana Tabora mpaka leo kuna mambo mengi sana yametokea ikiwemo Uchaguzi Mkuu ambao umewezesha Chama chetu kupata uwakilishi Bungeni na kuongoza Halmashauri ya Manispaa Kigoma Ujiji na uwakilishi kwenye Halmashauri za Wilaya 11 nchini kwetu. Chama chetu kimekua na sote kwa pamoja tujipongeze kwa hatua kubwa tuliyopiga. Katika kujipongeza kwetu kuna watu mbalimbali ambao kwa namna au nyengine waliweza wametufikisha hapa. Wengine wametangulia mbele ya haki kwa mfano mzee wetu Estomih Malla na wengine katika ngazi mbalimbali za chama. Viongozi wetu wa chama katika ngazi za kuanzia matawi, kata na majimbo; katika ngazi ya mkoa na Taifa walijitahidi kwa kadiri ya uwezo wao kukifanya chama kisonge mbele na kupanda mbegu. Nachukua fursa hii kuwapongeza wote kabisa na kuwashukuru kwa kazi kubwa mliyofanya. Kwa namna ya kipekee kabisa nampongeza Mgombea wetu wa Urais na Mgombea Mwenza wake kwa kuzunguka nchini nzima kukitangaza chama chetu na kukiweka katika ramani ya siasa nchini. 
Kazi haijaisha, lazima iendelee ili kuweza kutimiza malengo yetu ya kujenga siasa mpya katika nchi yetu, siasa za masuala na kuachana kabisa na siasa za matukio. Leo Halmashauri Kuu inakutana, pamoja na mambo mengine, itajadili na kupitisha Mpango Mkakati wa Chama wa miaka mitano. Timu yetu ya Watendaji wa Makao Makuu ya chama na Vikao vya Halmashauri Kuu tayari vimepitisha kwa upande wao na sasa ni zamu ya Mkutano huu wa Halmashauri Kuu kujadili na kupitisha Mwelekeo wa Chama chetu katika Miaka mitano ijayo. Kama myakavyoona, Kauli Mbiu yetu mpya inayopendekezwa ni SIASA ni MAENDELEO (Developmental Politics). Tunataka tujihangaishe na mambo ya wananchi, kero za wananchi, changamoto za wananchi na kushiriki nao kupata mawajawabu ya Changamoto hizo. Tunataka kila mahala ambapo Chama chetu kimepata uwakilishi kuongoza tofauti na vyama vingine; kuonyesha kuwa kweli tunataka kufanya siasa tofauti. Kila Mtaa ambao ACT Wazalendo ina Mwenyekiti au mjumbe, kila Kijiji ambacho tunaongoza na kila Kata ambayo tuna Diwani, lazima iwe tofauti kimaendeleo na kiuwakilishi. Kila Mamlaka ya Serikali ya Mtaa ambayo tunaongoza tuonyeshe tofauti na Mamlaka ambazo wenzetu wanaongoza. Tujikite kwenye mambo ya wananchi. Ndio Siasa ya Ujamaa inataka hivyo. Hali ya Nchi yetu Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii Kisiasa Hivi sasa nchi yetu ina Serikali mpya. Rais ameanza kazi kwa kasi kubwa katika eneo moja muhimu sana ambalo lilikuwa moja ya msingi mkubwa wa kuanzisha chama chetu – kupambana na ufisadi. Rais anaita ‘kutumbua majipu’. 
Chama chetu kilimwunga mkono Rais katika hatua ya mwanzo kabisa katika jambo hili. Ninaamini kuwa bado tutaendelea kumwunga mkono kwani ufisadi ni kansa na ni lazima kwanza kuizuia isisambae na kasha kuanza kuitibu kabisa. Hatua ambacho zinachukuliwa sasa na Rais ni hatua muhimu sana katika kuondoa ‘kutogusika’ kwa baadhi ya watu katika nchi yetu. Mnamkumbuka wakati tunazindua Chama tulizungumza kuhusu ‘cartels’ - vikundi maslahi ambavyo vimeshika uchumi wa nchi yetu. Hata hivyo, tunasema kuwa bado Rais hafanyi inavyopaswa. Bado Rais anapapasa suala la Ufisadi. Kuna mambo ya muda mrefu ambayo tunaendelea kama nchi kuyalipia Rais ameyakalia kimya. Mfano suala la Tegeta Escrow. Bado Mtambo wa IPTL upo chini ya matapeli na kila mwezi Serikali inawalipa matapeli hawa zaidi ya tshs 8 bilioni wazalishe au wasizalishe umeme. Hivi ndio vikundi maslahi ama cartels katika sekta ya Nishati ambavyo bila kuvibomoa Rais ataonekana anachagua katika vita hii. Suala la HatiFungani ya dola za kimarekani 600 milioni. Ni sawa kuwa kuna watu tayari wamefikishwa mahakamani kwa rushwa ya dola milioni sita. Lakini Serikali imefisha inaowaita madalali wa rushwa hiyo. Walioitoa rushwa hiyo Benki ya Standard ya Uingereza haipo mahakamani. Waliopokea rushwa hiyo maafisa wa Wizara ya Fedha hawapo mahakamani. HatiFungani hii ambayo Serikali imeanza kulipa riba yake ni ghali mno na imeongeza Deni la Taifa kwa kiwango cha shilingi 1.2 trilioni bila ya riba. 
Itakapofika mwaka 2020 ambapo tutakuwa tumemaliza kulipa deni hili, tutakuwa tumelipa zaidi ya shilingi 1.8 trilioni, shilingi bilioni 600 zaidi! Watanzania zaidi ya 2000 duniani kote wameweka saini kutaka Taasisi ya Rushwa kubwa nchini Uingereza ( SFO ) kufungua upya shauri hili na kuitaka Benki ya Standard iwajibike kwa ufisadi huu dhidi ya nchi masikini kama yetu. Rais wetu angeongoza Watanzania kukataa mikopo ya namna hii ambayo inafukarisha nchi ingekuwa ni hatua kubwa sana. Lakini TAKUKURU wanaona ni sifa kuweka ndani watu kwa bilioni 12 bila kutwambia watu watakaofaidika na bilioni 600 zaidi tutakazolipa katika deni hili. Ndio naama tunasema Rais na Serikali yake bado hawafanyi ya kutosha katika vita dhidi ya rushwa. Sio suala la kutumbua majipu tu, ni suala la kuweka mfumo madhubuti ambao utazuia rushwa kabisa na kama sio kuimaliza. Chama chetu cha ACT Wazalendo ni lazima kiendelee kuunga mkono juhudi zozote za kuondoa ufisadi nchini kwetu. Hata hivyo Chama chetu ni lazima kiendelee kukosoa Serikali pale ambapo tunapoona mambo hayaendi sawa. Tusiogope kuikosoa Serikali kwa hoja kwani kukozoa Serikali ni tukio muhimu sana la kizalendo. Narudia tusiogope kukosoa Serikali kila inapobidi. Hivi sasa Wabunge wa vyama vya Upinzani wamesusia Bunge kwa sababu kuu tatu. Moja ni Bunge kutoonyeshwa moja kwa moja na Televisheni ya Taifa na Televisheni Binafsi, mbili ni Matumizi nje ya mpango wa Bajeti iliyopitishwa na Bunge na tatu ni Serikali kutokuwa na ‘instruments’ kwa Mawaziri. Hoja hizi ni hoja za msingi sana. Ni Haki ya wananchi kuona moja kwa moja namna wawakilishi wao wanavyofanya kazi. Censorship ni moja ya dalili za kujenga udikteta nchini. Kwamba anayepaswa kuonekana moja kwa moja ni mtu mmoja tu; inakuwa kama Korea Kaskazini hivi! Hili ni jambo ambalo Chama chetu lazima kiungane na vyama vingine kulikemea kwani ukiliacha hatujui kitafuata nini. Kwamba Bunge lia studio zake nk, ni jambo la kuhadaa tu wananchi. Umeshawapa wananchi uhuru wa kuona Bunge moja kwa moja kwa miaka 10, halafu leo unawanyanganya? Mwalimu Nyerere alipata kusema “ jambo lolote linalowapa uhuru wananchi ni jambo la kimaendeleo”. Suala la gharama ni hoja dhaifu mno maana kampuni huru kama Azam TV na Startv walikuwa wanaonyesha bila hizo gharama za Serikali. Ni lazima kushikamana na wenzetu katika jambo hili. Suala la Matumizi kufanyika nje ya Mfumo wa Bajeti ni suala la kisheria. Bajeti inaongozwa na Sheria mbalimbali kama vile Sheria ya Fedha ( The Finance Act), Sheria ya Matumizi na Sheria ya Fedha za Serikali ( Public Finance Act). Kuna taratibu za Fedha za Serikali kuhamishwa kutoka fungu moja kwenda fungu jengine au ndani ya fungu husika. Katika Sheria zote hakuna mahala Rais amepewa mamlaka ya kuhamisha fungu lolote lile. Hivyo, hoja iliyotolewa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni kuhusu Wizara ya Ujenzi kuongezewa fedha mara 4 zaidi ya fedha ilizotengewa na Bunge ni hoja yenye nguvu sana. Izingatiwe kuwa Rais alikuwa Waziri katika Wizara iliyoongezewa Fedha hizo. Sio hoja ya kupuuza. Tukipuuza leo Rais anaweza kuamua kufanya lolote nan chi ikaingia kwenye taahruki. Lazima tumkatalie ili ajifunze kufanya kazi kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Nchi yetu. Mwalimu Nyerer alipata kusema “ Kuna mambo Rais akifanya, ya hovyo wananchi wakatae, awe Rais awe Rais square”. Dhana ya Mamlaka ( Power) ni dhana ngumu sana, ukilamba bila kuzuiwa utaendelea kulamba tu. Tumzuie Rais kupoka madaraka ya vyombo vingine vya dola. Tumwunge mkono kutekeleza madaraka yake ya Urais tu. Suala la ‘instruments’ ni suala linaloendana na suala la matumizi kubalishwa badilishwa. Kimsingi bila instruments Baraza la Mawaziri lina watu 2 tu – Rais na Makamu wa Rais. Kama Waziri Mkuu hana instruments hakuna Waziri Mkuu. Kama Mawaziri hawana instruments, hakuna mawaziri. Hivi sasa Serikali ina mawaziri hewa na hata maamuzi yao ni hewa. Instruments ni jambo la kisheria. Ndio zinatoa mamlaka kwa Mawaziri kufanya kazi. Hivyo kutokana na kutokuwa na Instruments kimsingi Rais ni Waziri wa Wizara zote nchini hivi sasa. Natoa wito kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ahakikishe Mawaziri wanapewa instruments ili waweze kuwepo kisheria na maamuzi yao yawe ya kisheria. Chama chetu kisikubali nchi kuendeshwa na mtu mmoja kwa jina la Rais. Nchi yetu iendeshwe kikatiba. Hata hivyo nataka kuwaasa Wabunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba Bunge la 11 lazima liwe tofauti na Mabunge yaliyopita. Mabunge yaliyopita yalikuwa na kazi ya kupambana na ufisadi kwa sababu Serikali iliyopita ilionekana kutofanya kazi hiyo vizuri. Bunge lilijipa kazi ya kutumbua majipu na kuilazimisha Serikali kutekeleza Maazimio ya Bunge. Hivi kazi hiyo ya kutumbua majipu inafanywa na Serikali yenyewe, inafanywa na Rais mwenyewe. Hivyo Bunge lazima litafute wajibu mpya katika kipindi hiki. Bunge na hasa wabunge wa upinzani lazima sasa kutazama njia mbadala za kuifanya Serikali iwajibike. Kwa mfano, ni dhahiri nafasi ya wazi kabisa ni katika ku ‘articulate’ mwelekeo wa nchi na kujenga mfumo madhubuti wa uwajibikaji. Ni lazima kubadilika na kubadili aina ya siasa. Tusifanye mambo yanayotarajiwa tutafanya kama kutoka tu bungeni halafu tunarudi tena. Kama Serikali inaenda kinyume na sheria, katiba na kanuni, kwanini tusifanye mikutano ya wananchi, bunge la wananchi ambapo tunajadili kwa uwazi mambo yanayotusibu. Tunaweza kutumia vizuri digital technology kuhakikisha ujumbe wetu unafika kwa wananchi bila kujali kama TBC wanaweka live au la. Ni lazima tuwe innovative katika Siasa. Tusifanye siasa za kila siku. Kiuchumi Serikali imewasilisha mpango wa Bajeti ambapo inatarajiwa kukusanya na kutumia zaidi ya shilingi trilioni 29 katika mwaka wa fedha 2016/17. Hii ni sawa na asilimia 28 ya Pato la Taifa ambalo sasa ni shilingi trilioni 98. Hata hivyo kwa fedha zetu za madafu inaonekana ni nyingi sana, kwani inatokana na kuporomoka kwa shilingi dhidi ya fedha za kigeni hasa dola ya kimarekani. Hata hivyo ni Bajeti kubwa yenye ongezeko kubwa hasa katika makusanyo ya ndani na mikopo ya ndani. Serikali itaongeza wigo wa kodi na hata kufikia wachuuzi wadogo wadogo kama wamachinga ili kuweza kupata fedha za kutekeleza Bajeti lakini pia Serikali itakopa fedha nyingi sana kutoka nje ya nchi, takribani shilingi trilioni 2 na pia itakopa sana kwenye benki za ndani na hivyo kufukuzana na wafanyabiashara katika mikopo ya ndani. Haya ni mambo ambayo ni muhimu kuyatazama katika muktadha mzima wa uchumi wa nchi yetu. Nina mashaka makubwa sana kama wachumi Serikalini waliikalia vizuri Bajeti ianyopendekezwa kwani kuna maeneo ambayo yanatia mashaka makubwa. Kwa mfano, Serikali inasema itaongeza mapato wakati mapato katika bidhaa zinazoingizwa kutoka nje yameanza kushuka. Kwa mujibu wa Taarifa ya Benki Kuu ya Mwezi Februari 2016, mizigo kutoka nje katika Bandari ya Dar es Salaam imeshuka kwa 40%. Katika mazingira hayo na kuzingatia kuwa tunategemea kodi ya forodha kwa asilimia 30 ya mapato yetu, mapato yatashuka tu. Vilevile Serikali imeshindwa kuzingatia kuwa Uchumi wa Dunia sasa unashuka na Uchumi wa Afrika unashuka.
 Tanzania sio kisiwa na inategemea sana uchumi wa Dunia na hasa nchi kama China ambapo uchumi wao umeporomoka sana. Chama chetu kiitake Serikali kuitazama upya Bajeti na kuelekeza fedha za kutosha katika maeneo yatakayowezesha uzalishaji wa ndani na hasa katika sekta ya kilimo ili kudhibiti kuporomoka kwa uchumi wa Dunia. Kijamii Hali ya wananchi ni mbaya, bidhaa zimeanza kupanda bei kuliko ilivyokuwa kabla ya uchaguzi. Chama chetu kijadili kwa undani hali ya maisha ya wananchi na kutoa tamko na mapendekezo ya namna ya kukabiliana na hali hiyo. 
Hali ya huduma za afya na elimu bado ni mbaya na hakuna mabadiliko makubwa ya ubora wa elimu na huduma za afya. Chama chetu kishauri Wabunge kuwatazama wananchi katika michango yao Bungeni ili Bajeti ya nchi yetu ihangaike na keri za wananchi. Hitimisho Ninawataka wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama muendelee kuwa wamoja na tuweze kujenga chama imara chenye kujali shida za wananchi. Tuna wajibu mkubwa na uwezo wa rasilimali fedha mdogo licha ya kwamba tuna rasilimali watu kubwa yenye kuweza kuleta mabadiliko. Ninawaomba tusivunjike moyo bali tutumie kila tulichonacho kujenga chama chetu ili kurejesha Ujamaa nchini kwetu. Nawatakia mkutano mwema. 
 Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mb Kiongozi wa Chama
Powered by Blogger.
Featured
Most Popular

Text Widget

Sample Text

Featured

About Me

Followers

TO DARE IS TO DO

TO DARE IS TO DO

OBAMA

OBAMA

INDIAN ICON

INDIAN ICON

Mwalim JK NYERERE

Mwalim JK NYERERE

TANZANIA ICON

TANZANIA ICON

Advertising

Advertising

Facebook

About Us

Ads

Definition List

Pages

Download

Blockquote

Recent Posts

Unordered List

ADVERTISE WITH US @GreatThinkerSays

Popular Posts

Videos